max
Administrator
      
Posts: 7
Joined: Mar 2009
Reputation: 0
|
this is a comment by an anonymous person on michuzi's blog...caught my att...
Watanzania tuacheni kuangalia mambo kwa kufuata dini. Huu si uungwana.
Watu wanatakiwa wateuliwe kwa kuangalia sifa zao. Hao jamaa hapo hakuna aliyeibuliwa kutoka kusikojulikana kama ilivyokuwa kwenye nafasi zingine hapo nyuma. Tuwe wakweli na tukubali kwamba kwa sababu za kihistoria tu, maeneo mengi nchini yenye shule ni yale yenye makanisa. Kadri nchi inavyosonga mbele ndivyo mambo yanavyojipanga kwa usawa. Si vizuri kulalamika. Wamishonari Wazungu walipokuja walijenga makanisa, hospitali na shule; Waarabu walijenga misikiti na maduka; hii imeathiri muundo wa taifa letu. Sidhani kama unaweza kulinganisha mathalani jinsi Uchagani kwa Wahaya kulivyo na mahali kama Kilwa Masoko au Kilwa Kivinje, hata mkoa wa Pwani, ukiondoa shule chache za serikali, zilizobaki zilijengwa na mapadri. Tukubali historia, tuache kulalama kwani hata viongozi wetu wa kwanza wa taifa karibu wote walisoma shule za Wazungu Wakristo.
Hakuna anayetuonea Waislamu, na ndiyo maana Nyerere alitaifisha shule za Wakristo ili Waislamu nasi tusome. Muulizeni Yusuf Makamba alisoma wapi, mwenyewe anasema kama si Wakristo asingefika hapo alipo. JK mwenyewe alisoma shule za Wakatoliki awali na alishawahi kusema hadharani.
Tujengeni taifa letu kwa misingi ya utu na maendeleo na umoja, tuache kabisa huu wimbo wa udini. Hakuna hata mtu mmoja atakayefaidika na vita vya kidini au mgogoro wa kidini. Tukomae, Tanzania hii ilijengwa na Nyerere na Karume bila kubaguana, tusiibadilishe.
Michuzi naomba uweke, mimi ni Mwislamu, lakini inabidi kuelezana ukweli. Tusiharibu nchi hata kidogo.
|
|
| 10-22-2009 04:52 AM |
|